*Ndege nne za kivita zatanda angani *Mkalimani uwanja FNB matatani JENEZA lililowekwa mwili wa Nelson Mandela, limewekewa vifaa maalumu vya
kiusalama vya kulifuatilia wakati likisafirishwa kutoka hospitali ya
kijeshi na hata litakaposafirishwa kuelekea kijijini kwake Qunu, kwa
ajili ya mazishi.
Helikopta za kijeshi aina ya Oryx, zipatazo
nne zikiwa na askari wa miamvuli, zimekuwa zikilifuatilia jeneza hilo
katika muda wote wa safari kuelekea Makao Makuu ya Serikali ya Union
Buildings.
Jeshi limesema kuwa, helikopta hizo zimewekewa vifaa
maalumu vya rada kufuatilia harakati zote za usafirishwaji wa jeneza
hilo, mpaka litakapoingia kaburini.
Msemaji wa Jeshi la Afrika Kusini (SANDF), Xolani Mabanga,
alipofuatwa kuhojiwa alisema, jeshi halijadili usalama wa vyombo vyake
katika vyombo vya habari na kusema kuna haja ya kuangalia mazishi ya
Mandela badala ya kujadili usalama.
Mabanga alisema bendera ya
Taifa hilo ambalo, limefunika jeneza la Mandela itaondolewa mara tu
baada ya mazishi ya Kiserikali kukamilika na kuvalishwa ngozi ya chui,
kabla ya kuingizwa kaburini.
“Ngozi ya chui inaonyesha utawala
na vile vile tutaweka ngao, ili kuonyesha kuwa mtawala huyo anajilinda
na anailinda nchi yake na ni mwana wa mfalme,” alisema Mabanga.
Alisema
kuwa Mandela atazikwa pamoja na ng’ombe dume ambaye atachinjwa na
kuingizwa pamoja kaburini na vile vile ng’ombe mwingine atachinjwa na
nyama yake italiwa, bila kuwekwa chumvi wala kitu chochote
0 Comments