Viongozi mbali mbali pamoja na raia wa Afrika Kusini
wanaendelea kutoa heshma za mwisho kwenye mwili wa aliyekuwa rais wa
kwanza mweusi wa Afrika Kusini Marehemu Nelson Mandela ambao umelazwa
kwenye ikulu ya Afrika Kusini mji Mkuu wa Pretoria, ambapo utalala hapo
kwa siku tatu.
Mwili ulichukuliwa katika msafara kutoka chumba cha maiti cha hosptali hadi kwenye jengo la Muungano.
Msafara wenye jeneza la Marehemu
uliondoka mjini katika Hosptali ya jeshi muda mfupi siku ya jumatano.
Jeneza lilibebwa kwenye gari maalum na kufunikwa bendera ya Afrika
Kusini.
Wananchi walijipanga kando kando ya barabara lilipopitishwa jeneza kama ishara ya kutoa heshma za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Msafara ulipita katika mitaa huku baadhi ya raia
wakikimbia pembeni kwenye mstari wa askari wa wanajeshi Mwandishi BBC's
Joseph Winter katika mji wa Pretoria amesema.
Wanajeshi waliobeba jeneza hilo walisonga hatua
kwa hatua hadi katika Majengo ya Muungano eneo alikoapishwa kuwa rais wa
kwanza mzalendo wa Afrika kusini 1994.
Wanachi, wakuu wa nchi walioalikwa na wageni
wengine wa kimataifa watapata nafasi ya kutoa heshima za mwisho kwenye
mwili wa marehemu aliyefariki alhamisi akiwa na umri wa miaka 95.
Wageni hata hivyo hawaruhusiwa kupiga picha.
Leo jioni wasanii mbali mbali wa Afrika Kusini
watashiriki katika tamasha maalum la kumuenzi Mandela na ambalo
wananchji wataruhusiwa kuhudhuria bila malipo.
Marehemu Mandela atazikwa nyumbani kwake katika kijiji Qunu katika jimbo la Cape Mashariki siku ya jumapili.
Maelfu ya raia wa Afrika ya kusini hapa jana
waliungana na viongozi mbali mbali duniani katika ibada ya kumbu kumbu
siku ya jumanne kama sehemu ya mfululizo wa maombolezo kifo chicho.
0 Comments