KUNA taarifa
zilizagaa kuwa msanii mkongwe wa vichekesho na maigizo nchini, Said
Ngamba ‘Mzee Small’ amefariki dunia.
Taarifa hizo ni za uongo na uzushi
maana mwandishi wetu ameongea na mke wa Mzee Small pamoja na Mzee Small
mwenyewe ambaye ni mzima kabisa! Mke wa Mzee Small anadai usiku kucha
hajalala maana alikuwa anapokea meseji za pole kutoka kwa watu
mbalimbali kuhusu taarifa hizo za uzushi.
Mzee Small mwenyewe amesema: "Mimi ni mzima kabisa japo bado nasumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi (stroke)"
0 Comments