Akiongea na mwandishi wetu, Irene amesema ni ngumu kuyajua maisha
ya mtu umwonapo barabarani lakini ukienda anakoishi ndiko utakapoujua
ukweli.
“Nimegundua kwamba asilimia kubwa
ya Watanzania wanaishi katika mazingira magumu, mabaya sana kuliko
unavyotegemea,”amesema Irene. “Unaweza ukakaa na mtu unapiga naye story,
kumbe kwake anakoishi ana maisha magumu kwelikweli,”ameongeza.
“Kwahiyo
mimi navyotembea hivi nakutana na vitu vingi na nimejifunza mengi. Mimi
nikikaa kwangu naona niko sawa, wengine wanakuwa hawana hata sehemu ya
kwenda choo, mtu akitaka kwenda chooni anachimba shimo kwa jembe.
Nimejifunza vitu vingi ambavyo nilikuwa sivijui vinaendelea katika hii
nchi.
Akiongelea changamoto za kipindi
hicho, Irene amesema wapo watu wamekuwa wakimpigia simu na kumponda kuwa
ameacha kujenga kwao na ameamua kusaidia watu wasio ndugu zake.
Changamoto nyingine ni kukutana na watu wanaojifanya wanashida kumbe ni
wasanii tu.
“Kuna nyumba moja tulienda yule mama akaelezea mpaka akalia lakini kumbe sinema tu, hana matatizo wala nini,” amesema Irene.
Ameeleza
kuwa wakati mwingine hukutana na watu wenye matatizo makubwa ambayo
wakimuelezea hujikuta yakimgusa kiasi cha kumliza na kushindwa kurekodi
kipindi.
“Mara nyingi kila nikienda sehemu
unakuta mtu ananihadithia mpaka nashindwa kushoot machozi yananitoka,
yaani kiukweli nakuwa naumia. Karibia scenes kibao nashindwa kushoot
sababu ya hiyo.”
0 Comments