Gari
la polisi likiwa limepakia maiti zaidi ya kumi zikipelekwa hospitali ya
mkoa wa Singida kwa ajili ya kuhifadhiwa na kutambuliwa.…
Gari
la polisi likiwa limepakia maiti zaidi ya kumi zikipelekwa hospitali ya
mkoa wa Singida kwa ajili ya kuhifadhiwa na kutambuliwa.
Moja
ya maiti ya ajali ya basi la Sumry iliyotokea katika kijiji cha Utaho,
Wilayani Ikungi mkoani Singida ikisubiri kupakiwa katika gari la polisi.
Watu 19 wa kijiji cha Utaho, wilayani Ikungi mkoani Singida jana wamepoteza maisha wakiwemo askari wanne
wa jeshi la polisi, baada ya kugongwa na basi la Summry wakati wakiwa
wanatoa msaada wa kumpakia marehemu kwenye gari la polisi aliyegongwa na
gari kubwa ambalo halikufahamika mara moja jana usiku.
Basi hilo la kampuni ya Sumry hufanya safari zake kati ya Kigoma na Dar-es-Salaam.
Taarifa zinasema Dereva wa basi hilo alikimbia mara tu na baada ya ajali hiyo na kulitekeleza basi hilo.
Mwandishi wa habari Elisante Mkumbo alifika
na kuwakuta wasafiri walionusurika wakiwa katika kituo cha polisi cha
Ikungi bila ya kujua hatima yao ya safari baada ya basi lao kuwakanyaga
na kuuwa watu 19.
0 Comments