NYOTA wa Bongo Fleva, Herry Samir
maarufu kama Mr. Blue amesema wasichana warembo, Wema Sepetu na Najma
ambao aliwahi kutoka nao kimapenzi kwa nyakati tofauti miaka ya nyuma,
walimfilisi kutokana na matumizi makubwa ya fedha alipotoka nao viwanja.
Akizungumza na paparazi wetu hivi
karibuni, Mr. Blue, msanii aliyeanza kupata umaarufu akiwa bado kijana
mdogo, alisema alilazimika kutumia fedha nyingi akiwa nao, kwani
vinginevyo wangemuona hana pesa, kitu ambacho hakuwa tayari kuona
kinatokea. “Mademu wengi walikuwa wanapenda sana
starehe, kila day (siku) wanataka twende kiwanja, ndiyo maana kama
unakumbuka niliyumba kimuziki. “Wanawake wengi niliotoka nao
hawajulikani, ila kuna Wema na Najma, ilikuwa ukizama nao dukani lazima
ufanye shopping (manunuzi) ya nguvu, kuanzia laki saba, nane na
kuendelea ili wakuone unazo na mademu wengi wakisikia tu umepiga shoo,
sms hazikauki kuomba uwatumie mawe (pesa),” alisema. Kuhusu maisha yake ya sasa, Mr. Blue
alisema yamebadilika sana, kwani hivi sasa ameoa mwanamke mwenye asili
ya Kiarabu na amejaliwa kupata mtoto mmoja, hivyo ni baba wa familia
ambaye pia anakaribia kumaliza mjengo wake siku si nyingi. Hata hivyo alisema mkewe siyo maarufu,
ana malengo na upendo kwani amekuwa akimuaga kila safari anayofanya na
kwamba hata yeye anaporejea nyumbani, hupokelewa vizuri. Mr. Blue ni mmoja kati ya wasanii wa muda mrefu ambao bado wanafanya muziki na wenye mashabiki wengi ndani na nje ya Bongo. GPL
0 Comments