Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akiwa Kajala Masanja.
KAMA kuna kitu kinakukwaza ndani ya moyo wako, siku zote ukikaa nacho kitazidi kukuumiza lakini ukiamua kumtafuta mtu ambaye umeshibana naye na kumsimulia, moja kwa moja utakuwa umeutua mzigo!
Hicho ndicho amekifanya Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kwa kuweka kweupe chanzo cha ugomvi wake na staa mwenzake, Kajala Masanja huku akijuta kumlipia mwanadada huyo zile Sh. milioni 13 za faini ili asiende jela miaka saba.
Akizungumza
na Ijumaa katika exclusive interview Jumanne iliyopita, Wema ambaye pia
ni staa mkubwa wa sinema za Kibongoalisema kuwa kuna mambo mazito
ambayo yamesababisha yeye kuingia kwenye gogoro kubwa na Kajala.Wema au
Beautiful Onyinye alisema kwamba mambo hayo ndiyo yamemsababishia
maumivu ya moyo na kutokwa machozi kila wakati.
“Leo
(anataja jina la mwandishi), ngoja nikuelezee kila kitu kinachohusiana
na mimi na Kajala juu ya tofauti zetu.“Naamini baada ya kusimulia kisa
na mkasa nitakuwa nimeutua huu mzigo mkubwa nilionao ndani ya moyo
wangu.
“Baada ya hapo sitapenda tena kuzungumzia ishu inayonihusu mimi na Kajala,” alianza kufunguka Wema.
UZINDUZI WA KIGODORO
Katika
maelezo yake, cha kwanza, Wema ni uzinduzi wa Filamu ya Kigodoro
uliofanyika hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem
jijini Dar ambapo yeye alisema kuwa alianza kuyaamini yale yaliyokuwa
yakisemwa na watu kuhusiana na Kajala.
Wema
alisema kabla ya tukio, akiwa saluni akijiandaa kwa ajili ya uzinduzi
huo, ghafla Kajala alimharibia ‘mudi’. “Unajua ile Saluni ya (anataja
jina la saluni) pale Kinondoni, ina sehemu mbili, juu na chini, sasa
mimi nilikuwa juu na Aunt (Ezekiel) tunatengeneza nywele.
“Niliposhuka
kwa ajili ya kuosha nywele, nikamuona Kajala, kwa kuwa nilikuwa
sijaonana naye siku nyingi na tayari maneno yalishaanza kuwa mimi na
Kajala tuna bifu, nikaona nioneshe kuwa sina bifu naye.
“Kweli
nilipiga makelele ya furaha nilivyomuona K, nikawa nakimbia kwenda
kumkumbatia, kiukweli niliishiwa nguvu baada ya kunikwepa na kusema
nooo…Wema usinikumbatie na kuanza kutoa maneno ya dharau eti
nitamchafua.
“Kusema
kweli niliishiwa nguvu na kuona kama vile kizunguzungu huku aibu
ikinijaa ghafla kwani pale kulikuwa na watu wengi, basi huwezi kuamini,
nilishindwa kujizuia nikajikuta namtukana, sikumbakisha.
“Wakati
namtukana alikuwa amekaa kwenye kiti cha kuoshwa, nikaenda nikamsukuma
na kumfukuza pale kwenye kiti ili nikae nioshwe, huwezi amini hali ya
hewa iliharibika ghafla kwani sikuwa na mudi tena,” alitiririka Wema.
SAFARI YA ARUSHA KATIKA SHOO YA MIRROW
Wema
alisema kuwa baada ya kutofautiana pale saluni, hakuwa na kinyongo,
safari ya Arusha ilipofika walikwenda kumsapoti msanii wao wa Bongo
Fleva anayesimamiwa na Kampuni ya Endles Fame Production.
Wakiwa
njiani, kwa mujibu wa Wema, yeye alikuwa hana fedha taslimu za kutosha
zaidi ya kubeba kadi zake saba za ATM tofauti hivyo alimwambia Kajala
ampe shilingi laki tatu kwa ajili ya watu kula na kunywa njiani pamoja
na matumizi madogomadogo.
Alisema Kajala hakuwa na shilingi laki tatu akampa shilingi laki mbili na elfu themanini.
Aliendelea
kutoa ya moyoni: “Tulipofika Arusha Kajala alimwita ndugu yake mmoja
anayeitwa Doli kisha akamwambia achukue fedha alizokuwa nazo akamuwekee
benki kwa sababu sikuwa na fedha na nilianza kukopa eti nilijishaua
kuandaa shoo nikitegemea fedha zake.
“Wakati
K anazungumza hivyo kulikuwa na watu watatu, mimi sina hili wala lile
nikamuuliza mtu mmoja mbona siwaoni, wamekwenda wapi?
“Ndipo
nikafungukiwa kuwa wananikimbia kisa nimemkopa K hizo laki mbili na
elfu themanini, kiukweli iliniuma sana, Kanalalamikia laki mbili? Tena
hakunipa bali alinikopesha?
“Nilijiuliza
amesahau mimi nilitoa Sh. milioni 13 kumlipia faini asiende jela miaka
saba? Nguo nikinunua nanunua sare, nywele sare, viatu sare, mapochi
sare, ninachokula na kunywa mimi ndicho hichohicho.
“Siku
zote wakati akiwa gerezani nguo, viatu, hereni yaani kila kitu nilikuwa
ni mimi, leo laki mbili na elfu themanini, niliyomuazima ananitangazia
kwa watu (anataja jina la mwandishi)?
“Iliniuma
sana basi palepale, nikaenda benki nikatoa Sh. milioni mbili, nikamlipa
fedha zake, nikakaa kimya nikijifanya sijui chochote kinachoendelea
kwani ningefanya chochote ningeharibu shoo na isingekuwa na maana yoyote
ya sisi kwenda Arusha.”
WAREJEA DAR, MAANDALIZI YA FILAMU YAKE YAANZA
Wema alisema waliporejea Dar, alimwambia Kajala kuwa kuna mtu aliyekuwa amempa stori hivyo alimuomba wafanye filamu wawili.
Alisema
kwamba Kajala alikubali na kusema kuwa atachangia Sh. milioni tano
katika bajeti ya filamu hiyo.Baada ya kusikia hivyo, Wema alisema
alifarijika, alipokwenda kumweleza ‘bebi’ wake, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’, naye Diamond akasema atatoa Sh. milioni tano hivyo jumla
itakuwa Sh. milioni kumi ikapita bajeti iliyokuwa imepangwa ya
Sh.milioni nane.
Anaendelea:
“Tukiwa katika maandalizi ya mwisho tuanze ku-shoot, K alinipigia simu
akaniambia hawezi ku-shoot kwani alikuwa na safari ya kwenda China labda
wa-shoot vipande vyake, nikamwambia basi aende akirudi tutatengeneza
nyingine.
“Baada
ya kuona hivyo ndipo nikamchukua Aunt tutengeneze filamu. K alipoona
nimemchukua Aunt, akanipigia simu na kuanza kuongea shiti.“Nilijiuliza
mbona mwenzangu amesahau ghafla wema wangu niliomtendea au kwa kuwa
tangu aanze vijisafari vyake vya kwenda China anapata
0 Comments