Hamisa Mabeto
MWANAMITINDO maarufu nchini, Hamisa Mabeto ametishia maslahi ya wasanii
wa kike wa Bongo Movie baada ya kujitosa rasmi kwenye tasnia hiyo na
kung’ara katika Filamu ya VIP akiwa na mastaa, Vincent Kigosi ‘Ray’ na
Jacqueline Wolper.
“Wasanii wajiangalie nafasi zao baada ya Mabeto kuingia kwenye filamu
maana ndani ya VIP amekamua sana na wasipokuwa makini atawasumbua
kutokana na mvuto ulionao,” alisema Ray.
Mabeto ametamba kwenye ulimbwende tangu mwaka 2010 alipoibuka mshindi wa shindano XXL Back to School Bash.
Mwaka 2011 alishika nafasi ya pili katika shindano kumsaka Miss Dar Indian Ocean na baadaye Miss Kinondoni.
Mwaka 2011 alishiriki Miss Tanzania na kufika hatua ya nusu fainali ya
michuano hiyo. Mwaka 2012 akafika hatua ya kumi bora kwenye Miss
University.
Hivi karibuni alipata ulaji wa kupamba kava la gazeti
0 Comments