MWANADAFADA mkali wa Bongo Movies,
Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amefunguka kuwa kwa sasa yupo tayari kuigiza
nusu utupu kwa sinema za nje ya nchi. Akipiga stori mbili-tatu na kona hii,
Batuli alisema kuwa muvi nyingi Bongo huwa zinafungiwa kwa kukosa
maadili na kwamba kama ikitokea nafasi akaitwa nje ya nchi kuigiza sini
hizo, atakuwa tayari. “Zamani nilikuwa nikiogopa kuigiza nusu
utupu. Wenzetu Nigeria wameendelea na ndiyo maana wanaigiza hata nusu
utupu, kama itatokea nafasi ya kuigiza huko (nje ya Bongo) nusu utupu,
nipo tayari,” alisema Batuli.
0 Comments