Jana ilikua ni siku ya furaha kwa msanii “Tiwatope Savage” maarufu kama ‘Tiwa Savage’ ambae alifunga ndoa na mme wake “Tee Billz” ambae walikua wachumba kwa muda mrefu. Kabla hawajawa wachumba Tee alikua na meneja wa Tiwa msanii huyo kutoka nchini Nigeria. Ndoa yao imefanyika Dubai na ilihudhuliwa na watu maarufu peke yake.
Katika sherehe waliyofanya usiku wa jana msanii ‘Bank W’ aliwazawadia gari jipya wanandoa hao. Unaweza tazama picha za kilichojiri katika harusi hiyo.
Gari Waliyopewa Kama Zawadi |
Profesa J amesema Diamond Platnumz, alilia machozi wakati anafanya chorus ya wimbo wake ‘Kipi Sijasikia’
Rapper huyo alikiambia kipindi cha Sunrise cha Times FM kuwa wakati Diamond anarekodi chorus hiyo yeye na Majani walishangaa kumuona hitmaker huyo wa ‘My Number One’ akibubijikwa na machozi ndani ya ‘booth’.
“Lakini
kilichotushangaza alipoingia booth ili arekodi chorus Diamond alikuwa
anaimba huku analia. Sisi tuko kwenye monitors huku tunamuangalia jamaa
upande wa pili kwenye booth tunamuona Diamond analia.
Alikuwa
emotional unajua ile…ilimgusa sana. Sisi tulikuwa tunashangaa mimi na
Majani ‘huyu jamaa analia nini?’ Lakini baadae tulimuuliza alituambia
‘nimefurahi sana katika maisha yangu kufanya kazi na Profesa Jay pamoja
na Majani, hilo moja.
Lakini
pili, mlivyoimba humu ndani vyote vinanihusu mimi…vimenitokea sana
katika maisha yangu na changamoto zote hizo’..so yale ndio yalitokea
studio.
Kiukweli hii ngoma ilikuwa blessed tangu studio na kila mtu alikuwa anasema ‘yeah men it’s on’, alisema Profesa J.
- See more at: http://www.farajimfinanga.com/2014/04/masikini-diamond-amwaga-machozi-studio.html#sthash.yBwpIFie.dpuf
0 Comments