Anakila sababu ya kuwa maarafu ndani na nje ya Bongo kutokana na mchango wake mkubwa katika sanaa wa uigizaji wa Afrika Mashariki.
Ana fahamika kama Mzee Majuto lakini kwa jina la serikali ni Amri Athumani aliwahi kutamba katika tamthiliya za mwanzoni kama “Fukara Hatabiriki” na kuweza kumpatia umaarufu mkubwa sana.
Mzee Majuto ambaye anaendelea kufanya vizuri katika ulimwengu wa filam za Kitanzania na hivi karibuni alijikuta anapata mashabiki wengi sana baada ya kucheza kwa ujuzi wa hali ya juu katika filamu ‘Narudi Kwa Mwanangu’, ‘Shikamoo Mzee’, hapa Mzee Majuto anatueleza sababu ya kustaafu kwake
“Naona umri wangu unazidi kwenda, kwakweli yanatosha yote niliyo yafanya ,naamua kuachana na uigizaji niwaachie vijana mimi tena nimeshakuwa babu yao lakini sito kaa pasipo kujishughulusha nimepanga kuanza shuguli za kilimo baada ya kustaafu sina muda mrefu kuwatangazia rasmi mashabiki wangu kuwa mimi naamua kupumzika nitatangaza rasmi ndani ya miezi miwili ijayo kwa sasa kuna mambo na malizia kwanza.
Naamini hakuna lolote litakalo badilika baada ya mimi kuondoka kwa sababu kuna vijana ambao wamebaki wana uwezo mkubwa sana katika uigizaji cha msingi wajitume kwa bidii na siyo kitu kingine.” Mzee Majuto
0 Comments