Mwanafunzi wa Eden Hilling College kilichopo mkoani Pwani aliyetajwa kwa jina la Atu Gabriel amefariki akidaiwa kujaribu kutoa mimba kwa kunywa vidonge.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani (RPC), Orech Mtei, katika
kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, alisema Jumamosi April 26 mwili wa
Atu ulikutwa katika chumba cha mwanaume aliyefahamika kwa jina la
Hafidhi ambaye anadaiwa kuwa mpenzi wake.
Kamanda
Mtei ameeleza kuwa polisi walikuta mwili wa marehemu ukiwa karibu na
vidonge alivyotumia huku akitokwa damu nyingi sehemu za siri na kwamba
polisi wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa Hafidhi ambaye alidaiwa kukimbia
baada ya tukio.
"Ni
kweli tukio hilo limetokea Jumamosi Aprili 26 mwaka huu eneo la Kwa
Mfipa baada ya jeshi letu kutaarifiwa kuwepo kwa mwili huo na polisi
walipofika na kufanya uchunguzi wake tulibaini marehemu alifariki dunia
kaika jaribia la utoaji wa mimba.....hata hivyo mwili bado upo
Hospitalini Tumbi kwa ajili ya uchunguzi zaidi," alisema Kamanda Mtei.
Kamanda
Mtei alisema mara baada ya kutokea kwa tukio hilo, kijana aliyetajwa
kwa jina la hafidhi ambaye inadaiwa alikuwa mpenzi wake alitokewa eneo
la tukio na jeshi hilo kwa sasa linamtafuta kwa ajili ya mahojiano zaidi
kabla ya kufikishwa mahakamani.
"Baada
ya tukio mtuhumiwa alikimbia na hadi sasa bado haijulikana alipo, jeshi
letu linaendelea kumtafuta popote alipo na mara baada ya kumpata
tutamuhoji na baadae atafikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua za
kisheri," alisema Mtei.
Secretary
wa Eden Hilling College ambaye hakutaka jina lake litajwe alieleza kuwa
mwanafunzi huyo aliaga chuoni hapo siku ya Alhamisi kuwa anakwenda
katika hospitali ya Mwananyamala kumuuguza wifi yake na kwamba
wamesikitishwa sana na habari ya kifo cha mwanafunzi huyo.
"Aliaga
vizuri tu siku ya Alhamisi kwamba anauguliwa na anakwenda kumuuguza
wifi yake aliyelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala lakini Jumamosi
ndio tukapokea taarifa za kifo chake! Hii inaonyesha huyu mwanafunzi
aliudanganya uongozi wa Chuo kitu ambacho hakikuwa sawa kabisa,"
Alisema.
Alisema hivi sasa uongozi wa Chuo unawasiliana na wazazi wake waliopo Makambaku kwa ajili ya kuja kuuchukuwa mwili wa marehemu.
Profesa J amesema Diamond Platnumz, alilia machozi wakati anafanya chorus ya wimbo wake ‘Kipi Sijasikia’
Rapper huyo alikiambia kipindi cha Sunrise cha Times FM kuwa wakati Diamond anarekodi chorus hiyo yeye na Majani walishangaa kumuona hitmaker huyo wa ‘My Number One’ akibubijikwa na machozi ndani ya ‘booth’.
“Lakini
kilichotushangaza alipoingia booth ili arekodi chorus Diamond alikuwa
anaimba huku analia. Sisi tuko kwenye monitors huku tunamuangalia jamaa
upande wa pili kwenye booth tunamuona Diamond analia.
Alikuwa
emotional unajua ile…ilimgusa sana. Sisi tulikuwa tunashangaa mimi na
Majani ‘huyu jamaa analia nini?’ Lakini baadae tulimuuliza alituambia
‘nimefurahi sana katika maisha yangu kufanya kazi na Profesa Jay pamoja
na Majani, hilo moja.
Lakini
pili, mlivyoimba humu ndani vyote vinanihusu mimi…vimenitokea sana
katika maisha yangu na changamoto zote hizo’..so yale ndio yalitokea
studio.
Kiukweli hii ngoma ilikuwa blessed tangu studio na kila mtu alikuwa anasema ‘yeah men it’s on’, alisema Profesa J.
- See more at: http://www.farajimfinanga.com/2014/04/masikini-diamond-amwaga-machozi-studio.html#sthash.yBwpIFie.dpuf
0 Comments