Wimbo
Maalumu wa Muungano ulioimbwa na wasanii 50 kutoka Tanzania ambao kwa
pamoja walikaa na kutengeneza wimbo huu,jina la wimbo huu unaitwa
Tuulinde umetayarishwa na maproducer wawili Ema the boy na Tuddy Thomas
kutoka Soround Sound Studio.
Wimbo
huu maalumu wa Muungano umeimbwa kutoka katika mahadhi tofauti tofauti
ya muziki wa hapa Tanzania kuna wa Bongo Flava, Taarab, Dansi, Hiphop
na muziki wa injili.
Inawezekana
ikawa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu,wasanii 50 tofauti
kuimba wimbo kwa pamoja,kwa ushirikiano mkubwa,wasanii hawa
wanatukumbusha umuhimu wa Muungano ambao ndio utanzania wetu.
Miongoni
mwa wasanii ambao utazisikia sauti zao ni pamoja na Kadjanito,
Mwasiti, Linah, Christina Shusho, Khadija Kopa, Frola Mbasha, Ommy
Dimpoz, Diamond, Josse Mara, Kalala Jr, Ali Kiba, Peter Msechu, Mrisho
Mpoto, Abdul Kiba, Mzee Yusuph, Angel, Mwana Fa, Nikki Wa pili, G Nako,
GodZilla, Madee, Asley, Shaa, Mandojo, Domokaya, Shilole na Roma
Mkatoliki.
- See more at: http://www.farajimfinanga.com/2014/04/sikiliza-na-download-wimbo-huu-kuhusu.html#sthash.CoHpvivQ.dpuf
0 Comments