MTANGAZAJI aliyepata
kuwika katika vituo mbalimbali vya runinga Bongo, Maimartha Jesse,
amedaiwa kuwauzia mastaa wa mjini dawa za kuongeza makalio.Habari za
moto kutoka kwa sosi wa kuaminika, zinasema kuwa Maimartha ambaye pia
huitwa Mai amefikia hatua hiyo baada ya yeye kutumia na kufanikiwa.
“Hamshangai
siku hizi kila staa anaonekana kuwa na makalio makubwa? Ni kazi ya Mai
hiyo. Anafanya hiyo biashara muda mrefu sana. Ni za kunywa na kupaka.
“Mbona hata
yeye ametumia dawa hizo muda mrefu sana? Ukimwangalia utagundua zamani
hakuwa na hipsi za kiivyo. Ni kwa sababu ya dawa,” alisema sosi huyo.
Akaongeza:
“Hata Lulu Semagongo (Aunt Lulu) ndiye aliyemsababishia kuwa na
makalio makubwa kwani wakati wako karibu alikuwa akimpa dawa hizo.”
Waandishi
wetu walifika dukani kwa Mai bila kujua kama ni waandishi na kuulizia
bidhaa hizo ambapo zilitolewa, wakapiga picha bila kugundulika.
Mai
akiwa hajui kuwa yupo mikononi mwa mapaparazi waliokuwa na njaa ya
habari, aliwaambia: “Ni dawa nzuri, mara moja zinarekebisha umbo na
unakuwa wa kuvutia. Kuna za shilingi 250,000 na 260,000 inategemea kama
ni vidonge au losheni.”
Mapaparazi
wetu walipompigia simu Mai baada ya kutoka dukani hapo na kumweleza
kuhusu uuzaji wa dawa hizo dukani kwake, alisema duka lake linauza
urembo wa aina zote kwa mastaa na wasio mastaa.
“Kama
nimetumia dawa za kuongeza makalio, nyie inawahusu nini? Kifupi duka
langu linadili na urembo wa aina zote,” alisema Mai akishindwa kufafanua
zaidi.
Lulu
alipovutiwa waya na kuulizwa kama makalio yake ni matokeo mazuri ya dawa
za Mai alisema: “Sijawahi kutumia dawa za Mai kwa ajili ya kuongeza
makalio.
Yangu ya asili lakini watu wakinipigia simu na kuniuliza dawa za kuongeza makalio huwa nawaelekeza kwa Mai.
0 Comments