MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd ameungana na Majaji wanawake Duniani, kulaani vikali kitendo cha Ugaidi cha utekaji watoto wa kike 200 wa Nigeria, kilichofanywa hivi karibuni.
Hayo aliyasema jana wakati akifunga mkutano wa 12, uliofanyika Jijini Arusha na kukutanisha Majaji wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani (IAWJ) kujadili changamoto wanazokumbana nazo wakati wa utekelezaji wa
kazi zao.
Alisema kuwa kimsingi Duniani kuna unyanyasaji ambao unaendelea kufanyika dhidi ya wanawake na watoto, hali ambayo Majaji wanawake wamekuwa mstari w ambele kupambana nao.
“Lakini mimi nawaunga mkono nanyi katika maadhimio yenu ya kupinga ukatili huu wa utekeaji wa toto wetu huko Nigeria, siyo ubinadamu na inapaswa kulaaniwa na kila mmoja,”alisema.
Aidha alisema Majaji wanawake wamekuwa mstari w ambele kufanya kazi zao kwa uadilifu na kuhakikisha haki inapatikana bila ubaguzi kwa kila
mtu.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Majaji wanawake Tanzania, (TAWJA), Jaji Engera Kileo, alisema katika mkutano huo wa siku nne, wameadhimia mambo mengi, ilakubwa ni azimio la kulaani kitendo cha wasichana wa Nigeria kutekwa ambao kimsingi hawana makosa yoyote ya kufanyiw
aukatili huo.
“Hawa wasichana tunawalaani waliowafanyia hivyo, sababu wanakosa haki yao ya msingi ya kuwa huru na tunaomba matatifa makubwa na Umoja wa Mataifa, vikiwemo vyombo vyao kuingilia sakata hili ili watoto hao wapatikane wawe huru,”alisema.
Alisema hakuna mtu yoyote mwenye akili timamu atafurahia kitendo hicho cha kigaidi na kinapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote na mataifa yote Duniani.
0 Comments