Advertisement

Responsive Advertisement

Endless Fame Film watoa kauli kuhusiana na ugomvi wa Wema na Kajala….


Nyota wa muvi za Kibongo, Kajala Masanja.
Kajala na Wema

Kampuni ya filamu ya Wema Sepetu, Endless Fame Films, leo imetoa kauli yake kuhusiana na ugomvi wa mmiliki wa kampuni hiyo na aliyekuwa rafiki yake wa karibu Kajala Masanja. 


Maneja wa kampuni hiyo, Martin Kadinda ametoa msimamo huo kupitia mtandao wa Instagram.

“Good morning all of You…. I just woke up Like “Hasiraless” kwakuwa hili vugu vugu la kutokuwa na maelewano mazuri kati ya Wema sepetu (myclient) na Kajala limekuzwa katika social networks basi na mimi naomba nitoe taarifa kutoka kwetu endless fame.

Katika urafiki kuna mengi yanajitokeza na endapo kutakuwa na hitilafu sehemu basi ni muhimu kupeana nafasi ili kila mtu aweze kujirekebisha na mwisho wa siku maisha yaendelee hilo ndo lililotokea baina ya hawa wawili. 

Lakini katika kipindi hicho cha so called mapumziko kuna mambo mengi yamejitokeza, yapo ya kweli na yapo yaliyotengenezwa na baadhi ya watu, kuna media coverage juu ya hawa wawili na wema sikumpa nafasi ya kuzungumza na chombo chochote cha habari kwakuwa nilijua litakuzwa zaidi… ila tulipoona shutuma zinazidi kuja upande wake akafanya interview na gazeti moja na kuelezea upande wake na mwisho alisema hana tatizo na kajala sema tu Kwa sasa anahitaji space…… tukawa tumefunga mjadala huo.

Endless fame(wema sepetu) haijawahi kutamka lolote swala la mahusiano ya kajala na mtu yoyote, EndlessFame haijawahi kudoubt urafiki wa kajala na any of her friends because tunaamini yale ni maisha yake binafsi na hayahusiani na kampuni ya wema au wema mwenyewe, kusaidiana katika matatizo haimaanishi tunammiliki… hapana hapana… 
Hili linaloendelea sasa sisi pia tumelisikia na kuliona kwenye social networks kama watu wengine wanavyoona.

Tunaumizwa na blogs na magazeti yanapoandika stori kama vile wanaushahidi kutoka endless fame au Kwa mtu wa karibu na wema. Team wema wote waliopo insta sijawahi kuona hata mmoja kati yao hivyo hakuna anayewatuma wala kuwashinikiza ila wao wanafanya kile kinachowapendeza and hatuwezi kuwakataza kwasababu ni maisha yao binafsi na ni mapenzi yao ya dhati Kwa wema.

Poleni Kwa wote mnaoumizwa na haya yanayoendelea ila nadhani tukazane na kazi zetu na maisha yetu maana haya ya instagram tuwaache huku huku ukiyasikiliza utashindwa kumwamini mama yako mzazi.”
Hivi karibuni Kajala alisema kutokana na jinsi ambavyo ugomvi wake na Wema Sepetu ulivyokuwa mkubwa, amefikia hatua anaigopa simu yake zaidi ya kupiga na kupokea.

Akiongea wiki hii, Kajala alisema amekuwa akiumizwa na jinsi anavyotukanwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na ugomvi huo. Kajala amesema ugomvi wake na Wema haujatokana na kile kinachodaiwa kuwa alimchukulia ‘bwana yake’ na kwamba umetokana na vitu vidogo ambavyo ni binafsi kwao. 

Alidai kuwa pamoja na ugomvi wao kusababisha na mambo ya kawaida, umekuzwa mno na watu pamoja na vyombo vya habari kiasi cha kuwafanya wajikute maaudui kweli.

Kuhusiana na tetesi kuwa alianza kumdharau Wema baada ya Miss Tanzania huyo wa zamani kuishiwa fedha, Kajala amesema amekuwa rafiki yake tangia enzi hana chochote. 

“Alikuwa rafiki yangu kabla hana kitu, kwahiyo kwamba nilianzisha urafiki na Wema kwasababu alikuwa na hela lakini sasa hivi hana hela mimi sio rafiki yangu tena, sio kweli,” alisema.

Kajala alikiri kuwa kukosana kwake na Wema kumeathiri maisha yake. “Inaniathiri sana kwasababu ni mtu ambaye nimemzoea, mtu ambaye tumefanya vitu vingi kwahiyo sometimes nikikaa nammiss,” alisema na kueleza kuwa ameshawahi kumtaka Wema wamalize ugomvi wao lakini ilishindikana japo alisema kwakuwa ugomvi ni wao wenyewe, ipo siku utaisha na watakuwa marafiki tena.

Post a Comment

0 Comments