.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza,
Valentino Mlowola, amesema mlipuko
unaodaiwa kutokea may 05, ulitokana na kitu
kinachosadikiwa kuwa ni bomu la
kutengenezwa ‘kienyeji’ ambao ulilipuka katika
vyumba vya Hosteli za Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (K.K.K.T), mtaa wa Gana
Amesema tukio hilo limetokea jana Jumatatu
Mei 5, 2014 saa mbili usiku, na kujeruhi mtu
mmoja ambaye hadi sasa anapatiwa matibabu
katika Hospitali ya Rufaa Bugando iliyopo jijini
humo.
Taarifa za awali kuhusu tukio hilo,
zinaonyesha kuna watu/mtu ambao waliweka
bomu hilo katika hosteli hizo na kupelekea
tukio hilo, ambapo hadi sasa Jeshi hilo
linaendelea na upelelezi na hakuna mtu yeyote
anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo
0 Comments