Msanii wa Bongo Fleva, Raheem Nanji ‘Bob Junior’.
MTOTO wa msanii wa Bongo Fleva, Raheem Nanji ‘Bob Junior’ ametajwa
kuwa ndiyo sababu kubwa ya kurejesha ndoa iliyovunjika ya msanii huyo na
aliyekuwa mkewe iliyovunjika miezi michache iliyopita
.
Akizungumza na mwandishi wetu, msanii huyo alisema kuwa kipindi chote
wakati ameachana na mkewe alikuwa akimkumbuka sana mwanaye ambaye
alikuwa akiishi na mama yake, Halima.
Raheem Nanji ‘Bob Junior’ akiwa na mwanaye.
“Wakati nimetengana na mke wangu kitu kikubwa nilichokuwa nikikimisi
kilikuwa ni uwepo wa mwanangu, nashukuru Mungu kwa sasa nimerudiana
naye,” alisema Bob Juniour.
0 Comments