Hatimaye Nay wa Mitego amezungumzia scandal iliyokuwa ikimhusu
mchumba wake aitwaye Siwema ambaye mwezi uliopita ilisambaa video na
picha kwenye mtandao wa Instagram inayomuonesha akivishwa pete na
pedeshee.
Maelezo kuhusu video/picha hizi yalisema:
“Siwema demu wa Nay Wa Mitego amevalishwa
pete ya uchumba na jibaba ( pedeshee ) linalomuweka mjini na ndilo
lililomnunulia magari mwanzo aina ya Verosa na baadaye Kluger halafu
Verosa akampa Nay wa Mitego, sasa hivi kamnunulia Lexus harrier…
Inasemekana Nay pia analelewa na huyo dingi maana amekubalije amegewe
demu na kuhongwa gari alilohongwa demu wake.”
Pia kupitia mtandao huo, picha za msichana huyo zinazomuonesha akiwa nusu utupu zilisambaa.
Akiongea kwenye kipindi cha So So Fresh cha Clouds FM Ijumaa hii, Nay alisema ni kweli Siwema alimkosea lakini amemsamehe.
“Mimi Siwema ni mwanamke ambaye nampenda
kila mtu anafahamu maybe ndio maana ilikuja kuwa tatizo. Kuna vitu
vilitokea mimi nilikuwa sifahamu kama nilivyosema kuna watu wakanifuata
wenye nia zao sielewi mtu alikuwa na nia gani wakiviweka Instagram na
kwenye mtandao. Mimi mwanamke wangu najua alinikosea.
Sikujua
kilichokuwa kinaendelea lakini hakuweka wazi. Ni kitu ambacho kilitokea
kabla ya mimi kuwa naye lakini hakuwahi kuniambia kwamba kilitokea mpaka
wakafikia hatua ya design hiyo, hilo ni kosa ambalo alinikosea.
T
uliyamaliza, mimi ni gangster ambaye na nina mwanamke ambaye nampenda.
Huwezi kumwacha mwanamke kwasababu ya kitu ambacho ni cha historia,
sidhani kama ni fair.
Pia ni mwanamke ambaye mimi nipo naye kwasababu
tunapendana halafu ni mwanamke ambaye ananielewa na tunaelewana na ndio
maana niliamua kumweka wazi kila mtu anamfahamu. Hata kama itakuwa
vyovyote vile, siwezi kumwacha hata siku moja.
Kweli ni kosa kubwa
ambalo linahitaji moyo kwaajili ya kumsamehe mtu lakini naamini
nimefunzwa kusamehe kwenye mahusiano, hili ni la kwanza acha lipite
mwenyezi Mungu atusaidie tuendelee kudumu. Mimi nipo bado na Wema na
maisha yanaendelea.”
0 Comments