Advertisement

Responsive Advertisement

HUYU NDIYE BINTI ALIYEAMBUKIZWA VIRUSI VYA UKIMWI NA MWANAMKE MSAGAJI!!


Zuwena ( sio jina lake halisi ), ni mwanamke wa kitanzania mwenye umri wa miaka 43. Kwa sasa mwanadada huyu anaishi na virusi vya ukimwi.

Mwanadada huyu anabainisha namna alivyo pata maambukizi ya VVU kwa kujamiiana na mwanamke mwenzake, ama kwa lugha nyingine, Zuwena anaeleza namna ambavyo mwanamke msagaji alimuambukiza v.v.u wakati wakiwa na uhusiano wa jinsi moja… Fuatilia kisa hiki cha kufundisha na kusikitisha.

“Nakumbuka ilikuwa mwezi wa kumi na mbili mwaka 2007, nilipata tenda ya u MC katika sherehe ya kumuaga binti wa jirani yangu kule Buza Cape Town. Sherehe hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa Mihogoni Pub kulekule Buza.

“Saa moja usiku nilikuwa nimeshafika ukumbini na kutoa maelekezo kwa wageni waalikwa, watu walikuwa wengi kiasi ambacho hata mama mwenye sherehe alifurahi kwa jinsi watu walivyo muitikia. Kama kawaida niliendelea na matangazo ya hapa na pale, watu walicheza na kufurahi.

“Muda wa chakula ulipowadia nilikaa pembeni nikiwa naangalia watu wanavyo kwenda kuchukua chakula. Ghafla alitokea mama mmoja mtu mzima kwa kumkadiria alikuwa na miaka kama 48 – 50 hivi.

“Alinifata pale nilipokuwa nimesimama na kuanza kutoa sifa za hapa na pale mara umependeza , mara unaongea vizuri, mara vazi ulilovaa limekupendeza, mwisho aliniomba namba ya simu akaniambia kuwa ana sherehe ya kumuaga binti yake kwa hiyo angependa niwe MC katika shughuli yake. “Kwa kweli mimi nilikuwa kazini, sikukataa kumpa namba yangu. Kesho yake alinipigia simu ya kunisalimia, kwa kuwa kiumri alinizidi nilimuamkia, ila nilichokisikia masikioni mwangu ni neno ‘ Ahsante baby ‘.

“Nilishituka lakini nikaona ni vitu vya kawaida , kadri siku zilivyokwenda tulizidi kufahamiana nilimwambia kuwa nina saluni yangu, alinitumia vocha na mwisho alliniambia anataka kuja kupajua ofisini kwangu, nilimuelekeza akawa anakuja kutengeneza nywele, akitoa 10,000/= nikimrudishia chenji ananiambia “ utakunywa soda “ , siku nyingine anafika ofisini kwangu ananipa hela anaondoka.

“Nikaanza kuwa na mawazo juu ya huyu mama lakini sikupata jibu. Siku moja akanipigia simu akaniambia anataka kufungua saluni yake, kwa hiyo angeomba tukutane Cape Town Bar tuongee mimi na yeye. Ilikuwa siku ya Jumapili, wateja walikuwa wengi alinisubiri kama saa moja akanipigia
kuniulizia nimekwama wapi? Nikamwambia bado nina wateja ,akaniambia funga saluni njoo nikulipe hela ya siku hiyo yote.

“Nilifika pale akaniagizia kinywaji na baada ya hapo akatoa shilinge 50,000/= . Nilishindwa kumuelewa huyu mama akaanza kunihoji naishi na nani, nikamwambia naishi na watoto wangu watatu, baba yao baba yao amefariki  miaka miwili iliyopita . Nikamuuliza saluni anataka kufungulia wapi?

“Akanijibu achana kwanza na mambo hayo tutaongea baadaye . Tuliendelea kunywa hadi saa mbili usiku nikamwambia nawawahi watoto wangu nyumbani akaniambia nitakupeleka na gari, kusema kweli sikuelewa nia yake ni nini hivyo hata nyumbani kwangu sikutaka apajue.

“Nilimuaga tena kwa mara ya pili akaniruhusu , kesho yake aliniletea viroba vya unga na mchele akavishusha saluni kwangu, akaniambia atanipigia simu kesho yake kuna kitu anataka kunieleza.

“Nilianza kupata hofu, ilibidi niwaeleze rafiki zangu wa karibu ,ushauri walionipa waliniambia usikubali kutoka naye kwenda popote mbali ya pale Buza kwa sababu nia yake hatuielewi.
“Kesho yake akafika pale bar akanipigia simu, nikaenda ila nikapanga na rafiki yangu mmoja anifuate pale . Alipokuja nilitoa hela ili nimuagizie kinywaji, Yule mama alinizuia akatoa hela na kumuambia muhudumu alete kinywaji ila alimuomba yule rafiki yangu akae meza nyingine.

“Kusema kweli alizidi kunichanganya, sikumuelewa.  Yule
rafiki yangu alikunywa bia ya kwanza na ya pili na akaja kutuaga akaondoka. Nilimtumia meseji kuwa asicheze mbali.

“Baada ya kama lisaa limoja hivi alipigiwa simu, akaniaga akatoa Sh. 10,000/= akanibusu akaondoka.  Yaani hapo ndipo alinifanya niwe na mawazo sana, nikaenda kuwahadithia wenzangu ….wengine wakasema labda ni msagaji, wengine wakasema ametokea kukupenda tu au anataka kaka yake akuoe.

“Kesho yake akaja na dereva mwanamke, binti mdogo mwenye umri kati ya miaka 20 au 25, akaniambia nimsindikize mjini nikamchagulie nguo za biharusi mtarajiwa.

“Tukaondoka wote hadi Kariakoo, akamwambia Yule dada apaki gari pembeni ili akajisaidie, Yule binti akajitambulisha kwangu kuwa anaitwa Angel, akaniuliza huyu mama mmeanza kufahamiana toka lini, nikamwambia yapata mwezi mmoja sasa.
“Nikamuuliza mbona unaniuliza hivyo akaniambia nilikuwa nakuuliza tu. Akaniuliza unajishughulisha na nini , nikamwambia nina saluni na ni MC, akaniomba namba ya simu, Yule mama alipokuja akatuuliza mlikuwa mnaongea nini? Mimi nikamjibu kuwa dereva wako ananiuliza ile saluni ni yangu au nimeajiriwa ?
“Tukaja mpaka mtaa wa Tandamti akamwambia apaki gari atusubiri, tukaanza kuingia madukani, badala ya kutafuta nguo ya bi harusi akawa ananiambia mimi nichague nguo niliyoipenda nikawa namkatalia , tukaja mpaka mtaa wa Agrrey kuna duka linauza nguo za kutokea usiku, tukaingia pale kuna nguo nzuri tuliikuta inauzwa 120,000/= akaniambia niichukue nikakataa, tulipotoka nje kuna kaka alikuwa anauza viatu simple akaniambia nichague nikaona nisimkatishe tamaa nikachagua naye akachagua , Mara ikaingia meseji kwenye simu yangu , meseji ilikuwa  inasema hivi “ Huyo mama unamtambua vizuri au haumtambui, ni msagaji mzuri pole Aunty nakuhurumia, “ by Angel .

“Kwa kweli nilishtuka nikahisi nazimia , akaniambia mbona umesoma sms ukaonekana umeshtuka . Nikamwambia kaka yangu amenitumia sms mtoto wake anaumwa sana.Akaniambia twende nikupeleke , akili yangu ilishahama, nilimuambia tu hapana acha niende nikapande daladala niwahi hospitali.

“Alitoa shilingi 10,000/= akanipa kama nauli, nilitoka speed mithili ya mshale, nilivuka mtaa wa uhuru, nusu nigongwe na gari, sikuamini macho yangu, nilifungua tena ile sms nikaisoma , ghafla akanitumia vocha ya sh. 5000/= na ujumbe uliosema “ I love you baby “…. Nilipofika nyumbani nikawapigia rafiki zangu simu nikawaeleza, walishtuka sana, wengine waliniambia namsingizia .

“Rafiki yangu Hawa akanishauri nibadilishe laini siku hiyo hiyo na pale saluni nisikae. Nikanunua laini mpya , nikaenda kutafuta kazi ya saluni Yombo pale kwangu nikaweka msichana.

“Nikamwambia mtu yoyote akiniuliza amwambie nimesafiri na simu sina. Na kweli huyo mama alikuwa anakuja mara kwa mara saluni kwangu kuniulizia , lakini hakupata mafanikio yoyote.

“Matokeo yake niliamua kuhama nikapangisha nyumba yangu nikahamia Tandika nyumbani kwetu. Nilicho hofia ni kwamba kwa sababu nilishakula pesa yake nyingi, angefikia kunitaka kimapenzi, matokeo yake ningemkatalia angeweza kunifanyia chochote….

JE   KITU   GANI  KILITOKEA? ILIKUWAJE  HADI ZUWENA AKAAMBUKIZWA  VIRUSI  VYA  UKIMWI  NA MWANAMKE  HUYU  MSAGAJI ?

Post a Comment

0 Comments