Producer wa Burn Records, Sheddy Clever ameonesha kutoridhika kabisa na kitendo cha kuikosa tuzo ya mtayarishaji bora wa mwaka kwenye KTMA huku wimbo alioutayarisha 'My Number One' ukimuwezesha Diamond kuchukua tuzo kila ulipotajwa.
Ingawa producer huyo aliikosa tuzo hiyo na kuona ndoto yake moja ya mwaka huu ikififia, ameiambia tovuti ya Times Fm faida nyingine kubwa aliyoipata katika muziki huu wa kizazi kipya.
“Muziki umenipa faida nyingi sana sasa hivi namiliki studio yangu mwenyewe ‘Burn Records’ iko Tabata na pia nina usafiri namaanisha gari, nina gari langu mwenyewe. Na nina vitega uchumi vingi vidogovidogo tu ambavyo vingine mwenyezi Mungu anasaidia.” Amesema Sheddy Clever.
“Muziki umenipa mafanikio makubwa sana, japo sio saana lakini Mwenyezi Mungu anasaidia.” Ameongeza.
Bado mtayarishaji huyo ana ndoto kubwa katika maisha yake ili amiliki vitu vikubwa lakini kwa sasa ndoto yake aliyoiweka wazi pia kupitia Instagram ni kumiliki gari la thamani wanalomiliki watayarishaji wakubwa duniani.
Sheddy amepost kwenye Instagram picha ya gari zuri la kifahari na kuandika, Wenda ipo cku ndoto zitatimia mungu ndio muweza wa yote katika dunia hii don give up
0 Comments