Advertisement

Responsive Advertisement

Home Slider Udaku Spesho Master Jay "Uchawi Bongo Flava Upo Nimewahi Kuona Msanii Anatokwa na Panzi Kooni" MASTER JAY "UCHAWI BONGO FLAVA UPO NIMEWAHI KUONA MSANII ANATOKWA NA PANZI KOONI"!!

Producer mkongwe wa muziki na mmliki wa MJ Records, Master J, amesema uchawi upo kwenye muziki na ameshawahi kushuhudia msanii wa bendi akitolewa panzi kooni iliyoingia kimazingara ili ashindwe kuimba.
Akiongea na kipindi cha The Cruise cha East Africa Radio jana, Master J amesema wapo baadhi ya wanamuziki wanaojihusisha na masuala ya ushirikina.

“Hivi ni vitu vya kawaida, huu ni utamaduni wetu,mimi sishangai wala sioni kitu chochote cha ajabu. Mimi nilianza kwa kurekodi muziki wa rap tu, lakini baadaye nikaanza kurekodi band, Taarab na mchiriku ndio maana nishasemaga nimeshawahi kuona kwenye band mtu anatoa panzi kabisa kutoka kooni, akafanyiwa maujanja ndo akaweza kuimba. Kusikia wasanii wa Bongo Flava wanajihusisha sio kitu cha ajabu kwani wao si ni Watanzania na Tanzania taka usitake utamaduni wetu ni uchawi, uchawi upo,kwahiyo mimi sishangai,” alisema.

Post a Comment

0 Comments