BAADA ya juzikati msanii wa filamu Bongo, Meya Shaban ’Aki wa Bongo’ kuvuta jiko na ndoa yake kuwa gumzo, mwenzake Nicholaus Ngoda ’Ukwa wa Bongo’ naye amesema anasaka mchumba ili aoe.
Akizungumza na Ijumaa juzi, msanii huyo mwenye umri wa miaka 28 alisema, kwa sasa hana mchumba ila anamtegemea Mungu kumuongoza ampate mke sahihi.
“Mwenzangu kaoa na mimi sina sababu ya kusubiri sana, nikimpata mke sahihi nami nitaingia kwenye maisha ya ndoa. Katika hili namshirikisha sana Mungu maana si unajua wanawake wa sasa walivyo?” alisema Ukwa.
0 Comments