VIJANA wawili waliokuwa katika pikipiki aina ya Boxer wamenusurika
kuuawa na wananchi walioamua kujichukulia sheria mikononi eneo la Kijitonyama baada ya
kumpora dada mmoja mkoba.
Vibaka hao walifanikiwa kumpora dada huyo aliyekuwa akitembea kwa
miguu akitokea Benki ya Access katika maeneo ya showroom ya Akachube
iliyopo Kijitonyama jijini Dar.
Wakati wa uporaji huo, alikuwepo msamaria mmoja aliyekuwa na gari
aina ya Toyota Carina aliyefanikiwa kuwasukumia mtaroni na gari lake
ambapo wananchi walianza kuwashushia kichapo cha kufa mtu.
Kipondo kiliendelea mpaka askari wa jeshi la polisi walipofika na kuwanusuru.
0 Comments