Msanii wa muziki na producer, Bob Junior amesema kuna uwezekano mkubwa wa kufanya kolabo na msanii aliyemtoa, Diamond Platnumz.
Akizungumza na Bongo5, Bob Junior aliyetayarisha nyimbo za Diamond
zikiwemo ‘Kamwambie’ na ‘Mbagala’ amesema kwakuwa yeye ndiye aliyemtoa
akiamua muda wowote wanaweza kufanya naye kazi.
“Kwa sababu nia bado ipo na sisi tupo hai hatuwezi kujua nini
kitatokea, siwezi sema natamani ni kijana wangu ambaye nimemtoa mimi
nikiamua siku nafanya naye nitafanya naye, haiwezi kuwa na ugumu,”
amesema Bob Junior.

0 Comments