Ukatili
wa kijinsia haukubaliki hata kidogo, wengine tunapambana usiku na
mchana kutokomeza vitendo hivi vya Ukatili na Udhalilishaji, cha ajabu
watu maarufu sasaivi wamechachamaa kuendekeza vutendo hivyo..
Mara
Dudubaya kampiga Mke wake, mara Tid kamtukana RayC, Mara Chidbenz
kampiga mzazi mwenzake, mara Ezden kampiga mkewe, mara Chidbenz kampiga
RayC!!!! jamani jaman jamani kwanini mnachukua uamuzi huo wa
kudhalilisha Wanawake???
ChidBenz,
Tid, Ezden na Dudubaya nyie ni vioo kwenye jamii yetu, kwahiyo si vyema
kufanya vitendo vya kuwapiga Wanawake na kuwadhalilisha…kwani nyie
hamkoseagi? kuna siku mmepigwa? sisi sote ni watu wazima kwa hiyo kama
tumeshindwana kila mtu anachukua 50 zake kwa Amani…..
Kuna
msemo unasema kwamba Mwanaume wa kweli hapigi Wanawake wala
kumdhalilisha Mwanamke kwa sababu Wanawake ni Mama zenu. vitendo
mlivyowafanyia hao Wanawake mngependa Mama Zenu wafanyiwe???
Kama wewe unajiskia kupigana basi ni vyema ukaomba pambano na Matumla,
Kaseba au Cheka ili tujue kama kweli wewe ni mpigaji..kinyume na hapo ni
kuonea Wanawake na kuwadhalilisha kijinsia….
Nawaheshimu
sana kama wasanii lakini naomba mjirekebishe tena kuanzia sasa muwe
mabalozi wa Kupambana na vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji kwa
Wanawake. na muwaombe radhi wale mliowapiga na kuwadhalilisha..
Nipo
tayari kushirikiana na nyie kuhakikisha kuwa tunatokomeza
vitendo vya kikatili na udhalilishaji kwa wanawake…..
Ney
wa Mitego naomba useme na hawa mastaa wenzako ambao naona hawajasikia
ule ujumbe wako kwamba Mwanamke hapigwi na mangumi na mateke…Waeleze
Mwanamke anapigwa na nini…
Nakuita pia Linex utukumbushe ule ujumbe wako kwamba ndoa haivunjwi na mwanamke pekee bali hata Mwanaume nae aweza vunja ndoa.
Sasa
inapotokea mmeshindwa kuelewana au kukubaliana haifai utumie Nguvu
dhidi ya Mwanamke wako.. Kama mkishindwana mnaachana kwa Amani,
msiachane na kutuachia Mangeu…
0 Comments