Jeshi la polisi mkoani Iringa limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya
wananchi ambao walivamia na kuanza kuchota mafuta kwenye lori la kubeba
mafuta baada ya kupata ajali.
Ajali
hiyo imetokea jana eneo la msitu wa serikali wa Saohil wilayani
Mufindi, katika kwenye barabara kuu ya Iringa –Mbeya ambapo watu wawili
walijeruhiwa kwenye ajali hiyo.
Polisi
wamelazimika kutumia mabomu kuwatawanya wananchi hao ambao walikuwa
wakiendelea kumiminika kutaka kuiba mafuta kwenye lori hilo ili
kuwaepusha na hatari ambayo ingeweza kutokea kama lori hilo lingeshika
moto.
Mashuhuda
wamesema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi ya mbele ya lori
la mizigo lililokuwa linatokea mkoani Mbeya na hivyo kukosa mwelekeo na
kuligonga gari la kubeba mafuta lililokuwa linatokea mkoani Iringa na
kuanguka.
Jeshi la polisi mkoani iringa limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo unaendelea.

0 Comments