
Katika tukio la kwanza lililotokea Idd
Mosi, wakazi wa maeneo ya Afrikasana, waliamua kuweka mtego na kumnasa
changudoa aliyekutwa na mteja wake wakimaliza haja zao uchochoroni,
wakiwa wametandika boksi chini.
“Yaani tumechoshwa na hawa machangudoa,
inafikia hatua tunashindwa kulala kwa sababu ya miguno yao ya kimapenzi,
hata watoto wanashtuka usingizini kwa sababu ya mambo hayo, ni hatari
kwani wanaweza kujifunza ufuska, tumeamua kuwanasa leo jamani na itakuwa
fundisho kwao,” alilalamika mmoja wa majirani hao.
Huku timu ya Operesheni Fichuo Maovu
(OFM) ya Global Publishers ikiwa ‘beneti’ na majirani hao, ilishuhudia
wawili hao wakikamatwa na kupewa adhabu ya kulowanishwa kwa maji ya moto
ambapo nguo zao zililoa chapachapa.
Wakati changudoa huyo akipewa adhabu hiyo
ili liwe fundisho kwa wenzake wanaokesha pembezoni mwa barabara ya
Shekilango, msichana mwingine anayedhaniwa kuwa alilewa kupita kiasi,
alikutwa akiwa amezungukwa na watu nje ya baa maarufu ya Corner.
Kundi kubwa la watu lilimzunguka mwanamke
huyo kutokana na vitendo vyake kuashiria alikuwa amelewa bwii, wengine
wakiamini alikuwa na mapepo hivyo kutaka kujua namna ya kumsaidia.
“Huyu dada jamani itakuwa majini yake tu
yanamsumbua, si unajua watu wengine majini yao hayapendezwi na ulevi
uliozidi kiwango, maana mtu mwenyewe haeleweki, tukimshika kumsaidia
anataka kuturukia sasa sijui tufanyaje,” alisikika kijana mmoja akisema.
Hata hivyo, baadhi ya vijana waliokuwa
eneo hilo walionekana kupanga mbinu za kumchukuwa msichana huyo na
kwenda kumfanyizia, kitu kilichoshtukiwa na mabaunsa wa baa hiyo ambao
walimpandisha kwenye Bajaj na kumkimbiza Kituo cha Polisi Mabatini
ambako baada ya askari kuwasikiliza, walishauri apelekwe hospitalini.
Alipelekwa Hospitali ya Palestina ambako baada ya kupimwa, alionekana kunywa pombe kali kupindukia, hivyo kuwekewa dripu.
Credit: GPL
0 Comments