MAHAKAMA ya kikatiba nchini Uganda imefutilia mbali sheria dhidi ya
wapenzi wa jinsia moja ambayo ilisababisha mataifa ya magharibi kuinyima
msaada.
Kadhalika sheria hiyo ilizua gumzo sana siyo tu Uganda bali duniani
kote ambapo mataifa ya magharibi yalilazimika kuingilia kati.
Mahakama ilisema kuwa mswada huo kabla ya kuidhinishwa kuwa sheria
ulipitishwa na wabunge ambao idadi yao haikutosha kupitisha mswada hivyo
ni kinyume na sheria.
Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, tayari vilikuwa vimeharamishwa
nchini Uganda, lakini sheria hiyo mpya pia iliharamisha hatua zozote za
kueneza mapenzi ya jinsia moja na wakati huu hata kuwajumuisha wanawake
wasagaji kama sehemu ya wapenzi wa jinsia moja.
Mataifa kadhaa ya magharibi yamesitisha msaada kwa Uganda hasa baada ya sheria hiyo mpya kupitishwa.
Chanzo: BBCSWAHILI
VIA eddy.blog
0 Comments