Gazeti la KIU Aug 1 2014
Kama sehemu ya vyanzo vyako vya habari ni mitandao kama vile website,
blogs, facebook, twitter na Instagram inawezekana hii stori ya Gwajima
ambae ni Muhubiri wa Injili kununua Helikopta uliiona hata zaidi ya mara
moja.
Hata hivyo Muhubiri mwenzake Askofu Zacharia Kakobe Aug 10 2014
amenukuliwa na gazeti la Nyakati na kuizungumzia hiyo Helikopta akisema
‘kitendo cha Gwajima kununua helikopta kwa ajili ya kazi zake za Injili
kinastahili kufurahiwa na Wakristo wote wa kweli, tujifunze
kupongezana.. nampongeza sana’
‘Kumiliki kwake Helikopta kutachangia katika kufuta dhana potofu
ambayo imedumu kwa muda mrefu ya kuyaita Makanisa ya kilokole…. makanisa
ya vichochoroni, Helikopta sio starehe na hata muundo wake sio wa
starehe bali ni kazi, itamwezesha pia kufika maeneo ambayo gari sio
rahisi kumfikisha kutoa neno la Mungu’ – Kakobe
Kuhusu
Askofu Kakobe kununua Helikopta yake, amesema >>> ‘mimi sio
mtu wa mashindano na pia kila mtu anakwenda sawa kutokana na ono
aliloitiwa, haya sio mambo ya kushindana… hicho ndicho kinacholeta shida
mara kwa mara, Gwajima ana Helikopta ni kwa manufaa ya Ufalme wa Mungu,
mimi nina chakwangu ni kwa utukufu wa Mungu, hakuna haja ya kuigana’
credit:
Millard Ayo
0 Comments