KLABU ya Manchester City
imefanikiwa kukamilisha usajili wa beki Eliaquim Mangala kutoka klabu
ya Porto kwa ada inayokadiriw akufikia paundi milioni 32. Beki huyo wa
kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 alikaribia kujiunga na Cit
Januari mwaka huu. Meneja wa City Manuel Pellegrini amesema mchezaji
huyo bado anaweza kukua zaidi na kuwa mmoja wa mabeki bora barani Ulaya
kutokana na uwezo mkubwa alionao. Pellegrini aliendelea kudai kuwa
anategemea beki huyo anatozoea haraka mikikimikiki ya Ligi Kuu kutoka
nguvu na kipaji cha hali ya juu alichonacho. Mangala alikuwemo katika
kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kilichoshiriki michuano ya Kombe la
Dunia nchini Brazil lakini hakucheza mechi hata moja.
0 Comments