Advertisement

Responsive Advertisement

MANSOOR HIMID AKAMATWA ZANZIBAR, AKUTWA NA BUNDUKI AINA YA SHOTGUN NA BASTOLA


ALIYEKUWA mwakilishi wa CCM wa Jimbo la Kiembe Samaki, Mansour Yusuf Himid, amekamatwa na Jeshi la Polisi Zanzibar. 

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Zanzibar, Salum Msangi, alisema Himid alikutwa na bunduki aina ya Shotgun na bastola.

Himid ambaye siku za hivi karibuni alitangaza kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF) pia alikutwa na risasi za bastola 295 kunyume na taratibu zinazomtaka mtu anayemiliki kihalali awe na risasi 25.

Alikutwa pia na risasi za shotgun 112 wakati sheria zinataka mtu anayemiliki kihalali silaha hiyo awe ana risasi 50.

Kamanda Msangi, alisema kama Mzanzibar atakuwa na silaha atatakiwa apewe kibali na polisi, lakini Himid hakuwa nacho.

Hata hivyo, taarifa zilizokuwapo kwenye mitandao ya kijamii zilibainisha kuwa Himid alikuwa akishikiliwa katika Kituo cha Polisi Kati kwa tuhuma za kukutwa na silaha na huenda akaunganishwa katika kesi za ugaidi.

Himid aliyewahi kuwa waziri mwandamizi katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK) chini ya Rais Ali Mohammed Shein na hapo kabla chini ya Amani Karume, alifukuzwa uanachama wa CCM Agosti 26, mwaka jana kwa madai ya kukisaliti chama chake.

Mwanasiasa huyo anayedaiwa kuwa ni shemeji yake Rais Karume, kwa muda mrefu amekuwa akisifika kwa kuikosoa Serikali ya CCM na watawala wake.

chanzo:tanzania daima

Post a Comment

0 Comments