Mbunge wa Jimbo la Mbozi magharibi Mh. David Silinde (CHADEMA),
amewaeleza Wananchi wa jimbo lake maendeleo
aliyoyafanya toka alivyoingia madarakani akiwa na lengo la Wananchi kuendelea
kukipenda chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na kuakikisha
Wanachukuwa Madaraka tena 2015.
Hayo aliyasema katika mkutano wa Hadhara ambao ulifanyika
katika kituo kidogo cha mabasi Sogea katika mji mdogo wa Tunduma Uliopo jimboni
hapa, ambapo alianza kwa kueleza vitu ambavyo amefanya katika jimbo
hilo kuwa ni Ujenzi wa shule za msingi sita ambazo na yeye alichangia milioni 300
toka mfukoni kwake kwa ajili ya ujenzi huo mpaka kukamilika
Pia Silinde alisema kuwa baada ya kumaliza ujenzi huo aliomba
Madawati katika Benki ya NMB akapewa madawati 90 ambayo aligawa
madawati 15 kwa kila shule, vilevile kisima
ambacho kinatoa maji yenye ujazo wa lita laki moja na sabini kwa ajili ya usambazaji
katika mji wa Tunduma
Aliendelea kwa kusema kuwa wamejenga Daraja ambalo liligharimu milioni 48 kutoka Shule ya msingi Majengo Mpaka Msasani na watu
wanapita kwa raha tofauti na zamani walikuwa wanasumbuka katika uvukaji.
Pamoja na hayo alisema kuwa alitoa milioni 16 kununua
magodoro ambayo aliyasambaza katika vituo vyote vya Afya katika jimbo hilo,
Akijibu swali la Benard Mwashirindi ambalo aliuza "Utatusaidiaje Wanamomba
kwa kuwa hatuna Viwanja vya michezo vya kisasa?", Silinde alimjibu kuwa
maeneo yote waliokuwa wameyatenga kwa ajili ya viwanja yote yamejengwa na watu
ila kuna maeneo mengine ambyo yametengwa ambayo yapo Chapwa ila hawawezi kuanza
kujenga kwasababu hawajalipa fidia za wamiliki wa viwanja hivyo.
Akiendelea kutoa ufafanuzi juu ya viwanja hivyo alisema kuwa
Halmashauli ya Wilaya ya momba imetenga shilingi 404 milioni kwa ajili ya kilipa
fidia ndiyo waendeleze michezo huku akiwahakikishia Wananchi kwa kusema kuwa suala hilo lilikuwepo toka mda mrefu
Alimalizia
kwa kusema kuwa maeneo hayo yametengwa kwa ajili
ya Ujenzi wa Halmashauri na wameshaongea na TBA pia katika maeneo hayo
baadhi ni kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha ufundi, mahakama, na hospitali
kubwa ya
Wilaya.
0 Comments