Msanii anayefanya vizuri kunako tasnia ya filamu Bongo, Rayuu Bagenzi 'Rayuu' ambaye amewahi kukumbwa na skendo kibao ikiwemo kupiga picha za nusu uchi pamoja na kuonyesha michoro ya tatoo katika sehemu zake nyeti amedai kuwa amelazimika kubadili mwenendo wake hivyo kuomba radhi kwa kuikwaza Familia yake, ndugu, jamaa na marafiki
Rayuu
aliamua kuchukua maamuzi hayo baada ya kuona anakoelekea si
kwema hasa katika kujenga msingi wa maisha yake na sanaa kwa
ujumla.....Hata hivyo msanii huyo alikana kusambaza picha zake
za utupu na kushikilia msimamo kuwa picha hizo zilivujishwa na
watu wake waliokuwa na nia ya kumchafua....
"Naiomba
radhi familia yangu, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na jamii
nzima kwa yote niliyofanya.Nimeamua kubadilika na kujitenga na
watu wabaya ambao hawanitakii mema. Mimi ni mtu mzima hivyo
najua haya ninayoyafanya yatakuja kunigharimu baadae," alisema Rayuu.
Aliongeza
kuwa skendo nyingi chafu zilimdhalilisha na kuleta fedheha
katika familia yake na kwamba hahitaji tena kutokea kwa hali
hiyo
0 Comments