Afisa afya zahanati hiyo, Costansia Mpangile aliwaeleza waandishi wa
habari kituoni hapo kuwa hali hiyo inatokana na kukosekana kwa umeme.
Mpangile alisema wanalazimika kutumia tochi wanazotoka zao binafsi
kwa ajili ya kupata mwanga wakati wa kuwahudumia wajawazito wanaohitaji
kujifungua kwa dharura usiku na wagonjwa wanaohitaji kushonwa majeraha.
Alisema kuwa hali hiyo inatishia usalama wa utoaji wa huduma na hasa
ikizingatiwa kuwa zahanati hiyo imekuwa ikipokea wagonjwa kutoka vijiji
mbalimbali vya ndani na nje ya kata hiyo.
“Kama umeme ungekuwepo ungesaidia tuwe na majokofu ya kuhifadhi
chanjo na kuondoa mzigo kwa wananchi kufuata huduma hizo makao makuu ya
tarafa kwenye kituo cha afya ambacho kiko mbali.
“Kwa siku tunapokea wagonjwa 30 hadi 40, wakati wa usiku ndio inakuwa
ngumu kutoa huduma kwani umeme hakuna na hivyo hatari sana kwa wagonjwa
wetu,”alisema.
Alisema iwapo serikali itatilia mkazo changamoto hiyo kwa haraka,
kuna uwezekano mkubwa wa kusaidia kupunguza vifo vya kina mama
wajawazito na watoto, sambamba na kuboresha zaidi utoaji wa huduma.
Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara, baadhi ya wananchi wa
Kivukoni, Sofia Msalata na Salum Mnyambule walisema pamoja na kujisajili
kwenye mifuko ya afya ya jamii, bado huduma zinazotolewa
katika zahanati hiyo haitoshelezi.
Naye mbunge wa Ulanga Magharibi, Dk. Haji Mponda, alisema tayari
waliisukuma Serikali kuona changamoto hiyo na ilitenga sh. milioni saba
kwaajili ya kufikisha umeme katika zahanati hiyo lakini kinachokwamisha
hivi sasa ni utaratibu wa mfumo wa malipo ya serikali.
credit.eddy.blog
0 Comments