Wema na Loga kocha mkuu wa Simba |
Mzungu aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Zdravko Logarusic ‘Loga’ anadaiwa kuingilia penzi la mwigizaji Wema Sepetu.
Ishu hiyo imebumburuka ikiwa ni siku chache tangu Diamond atangaze kuwa hayupo tayari kuoa akidai atashuka kimuziki.
KUMBE ALIMZIMIA KITAMBO
Kwa
mujibu wa chanzo makini, Mcroatia huyo alimzimia Wema mara tu baada ya
kutua nchini Desemba, mwaka jana na kumuona mlimbwende huyo ‘akishaini’
kupitia vyombo vya habari, akajiwekea nadhiri kwamba lazima ampate.
CHANZO CHATIRIRIKA
“Loga
alimzimia kinoma Wema baada ya kumuona kwenye vyombo vya habari na
kuanza kufuatilia baadhi ya filamu zake ambazo zilikuwa zilimkonga moyo
kila alipozitazama.
“Baada ya kuvutiwa naye, mtu mzima (Loga) akaanza kutafuta mbinu za kumuimbisha Wema,” kilidai chanzo.
Chanzo hicho kilidai kwamba baada ya kocha huyo kupata wazo la
kumtongoza Wema, alianza kumsaka katika viwanja ambavyo aliamini mrembo
huyo anatembelea ili aweze kufanikisha azma yake ya kuonja penzi la Wema
AMSAKA NYUMBANI KWAKE
Ilisemekana
kuwa mara kadhaa alishafanya jitihada za kumfuata Wema nyumbani kwake
Kijitonyama jijini Dar lakini kila alipotia mguu, hakufanikiwa kuonana
na mrembo huyo.
Hata hivyo, ilisemekana kwamba Loga hakukata tamaa kwani alionekana kudata kadiri siku zilivyozidi kuyoyoma.
“Jamaa alipiga sana misele pale Kijitonyama lakini bahati mbaya, misele
yake haikuzaa matunda lakini kwa kuwa alikuwa na nia, hakukata tamaa,
aliendelea kumsaka katika viunga mbalimbali ambavyo aliamini Wema yupo,”
kilidai chanzo hicho.
ZALI LA MENTALI
Kikizidi
kumwaga taarifa, chanzo hicho kilibainisha kuwa jitihada za Loga
kukutana na Wema zilizaa matunda Aprili 22, mwaka huu maeneo ya Mwenge
ambapo bila kutegemea, wawili hao walikutana kila mmoja alipokuwa katika
mizunguko yake ya kikazi.
“Ilikuwa kama zali tu siku hiyo, Wema alikuwa katika ofisi moja hivi
ambayo alikuwa akifanya shughuli zake za kikazi lakini wakati huohuo
Loga naye alitia timu katika ofisi hiyo kwa shughuli zake za kikazi
ndipo ilipokuwa golden chance,” kilizidi kudai chanzo hicho ambacho ni
mtu wa karibu wa Wema.
Diamond |
NDOTO ZAANZA KUTIMIA
Chanzo
hicho kilizidi kutiririka kuwa, mara baada ya wawili hao kukutana,
pointi ya kwanza muhimu kwa Loga ilikuwa ni kubadilishana namba na
mrembo huyo kisha kufanya naye mazungumzo ya kawaida kwa dakika kadhaa.
Ilisemekana kwamba, siku hiyo Loga alionekana mwenye furaha kwani licha
ya kubadilishana namba za simu, ilielezwa kuwa walipata fursa ya kupiga
picha za pamoja na kutumiana kupitia simu zao hivyo ukaribu wao kuanza
kushamiri kuanzia hapo.
AANZA KUIMBISHA
Ilidaiwa
kuwa kitendo cha kocha huyo kupata namba ya Wema ilikuwa bahati kama
kuokota madafu kwenye miti ya miembe, haraka alianza kutuma maombi ya
penzi pasipo kufunguka moja kwa moja kisha badaaye alifunguka kabisa.
“Alianza kwa salamu, akawa anachombezachombeza na maneno ya mitego
ambayo mtu mzima ukitumiwa meseji kama hizo unajua kabisa kuna kitu mtu
anakitaka kutoka kwako.
“Alipoona Wema haelekei mtegoni, akaamua bora
kufunguka laivu, akamtumia meseji zinazoeleza hisia kali ya mapenzi,”
kilidai chanzo hicho.
USHAHIDI HADHARANI
Ili kuupata ukweli wa madai hayo, paparazi wa Globalpublishers kupitia gazeti la Risasi Jumatano alianza kuchimba undani wa sakata hilo ambapo kwa kutumia njia za ‘kiintelejensia’, alifanikiwa kunasa meseji (SMS) zilizotoka kwa Loga kwenda kwa Wema ambazo zilionesha dhahiri kwamba kocha huyo amedatishwa na staa huyo wa filamu na kuomba hifadhi ya kimalovee.
Ili kuupata ukweli wa madai hayo, paparazi wa Globalpublishers kupitia gazeti la Risasi Jumatano alianza kuchimba undani wa sakata hilo ambapo kwa kutumia njia za ‘kiintelejensia’, alifanikiwa kunasa meseji (SMS) zilizotoka kwa Loga kwenda kwa Wema ambazo zilionesha dhahiri kwamba kocha huyo amedatishwa na staa huyo wa filamu na kuomba hifadhi ya kimalovee.
Meseji
hizo zilikuwa zikisisitiza kwamba Loga anamhitaji Wema lakini mtoto wa
kike alikuwa mzito kumkubalia mzungu huyo ambaye sasa amesitishiwa ajira
yake na uongozi wa Msimbazi, mwishoni mwa wiki iliyopita kutokana na
makosa mbalimbali.
WEMA ANASEMAJE
Ili kujiridhisha zaidi, Globalpublishers ilimvutia waya Wema na kumuuliza kuhusiana na uhusiano wake na kocha huyo.
Ili kujiridhisha zaidi, Globalpublishers ilimvutia waya Wema na kumuuliza kuhusiana na uhusiano wake na kocha huyo.
Paparazi: Tumesikia Loga anakuimbisha, vipi umemkubalia au vipi?
Wema: Mh! Nani kakwambia?
Paparazi: Nijibu swali langu maana hata ushahidi wa meseji alizokutumia akionesha anakuhitaji, tumeziona na tunazo.
Wema: Kwani kuna tatizo akinihitaji? Si mwanaume, ana haki ya kupenda kama walivyo wengine lakini ishu ni kumkubalia.
Paparazi: Kwa hiyo wewe umemkubalia?
Wema: Aaaa wapi, sipo interested na wazungu hata kidogo by the way mimi nina baby wangu Diamond.
MADAI MENGINE
Wakati
huohuo, mtu wa karibu na kocha huyo amepenyeza madai kuwa Loga alipanga
kumhamisha Wema na kwenda kuishi naye nje ya nchi lakini haikujulikana
mara moja kwamba ni nchi gani achilia mbali kama ilikuwa ni ‘gia’ ya
kumpata mwigizaji huyo.
Alipotafutwa Loga ili kuzungumzia madai hayo, hakupatikana mara moja
hivyo jitihada zinaendelea, tega sikio kwenye magazeti ya Global.
Kama
hiyo haitoshi, pia Loga anadaiwa kutoka na mwigizaji Yvonne-Cherry
Ngatwika ‘Monalisa’, madai ambayo mwigizaji huyo ameyakanusha vikali.
source: Globalpublishers
0 Comments