Msanii
wa Filamu za kibongo Salma Jabu ‘Nisha’ amedai kuwa hamjui
mwanaume atakayeweza kuitwa baba wa watoto wake kwani kila
mwanaume anayemtaka kimapenzi huwa haamini kama anaweza kutimiza
hilo katika maisha yake ya mapenzi…..
Nisha
alisema hivi sasa ni mapema sana kuwa na mawazo ya namna
hiyo kwani bado anatafakari, na kudai hawezi kuweka asilimia
nyingi wakati bado yeye ni kijana na anatafuta hela kwa sasa
na si familia…..
“Nahitaji kuweka akili chini kwa sababu ishu ya kuzaa au kuwa na mwanaume ambaye anaweza kulea watoto si kitu kidogo, ni lazima akili yangu itulie na ifanye maamuzi mazuri kwa ajili ya maisha yangu vinginevyo naweza kulia kwa sababu sitakuwa na maamuzi sahihi ambayo yatanifanya niishi kwa raha,” alisema Nisha.
Muigizaji
huyo tangu aanze kupata jina amevurugwa na wanaume kadhaa
kimapenzi akiwemo staa wa bongo fleva Ney wa Mitego, ambaye
uhusiano wao ulionekana kama wa kutaka kiki kabla ya kutemana
ghafla
0 Comments