Mkali
wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka amesema kuwa katika maisha
yake amejiwekea utaratibu wa kujiheshimu ndio maana anaheshimika
na watu wa kila rika , tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma
alipokuwa anakumbwa na skendo za mara kwa mara….
Akizungumza
na mwandishi, Ndauka alisema kuwa akili aliyonayo sasa ni ya
kikubwa na anaangalia malezi ya mwanaye ambaye naye atapenda
akuwe akiwa na maadili mema ambayo yatamsaidia kujiepusha
kuingia kwenye dimbwi la vijana wenye tabia mbaya….
“Najiheshimu ndo maana naheshimika, ukiwatafuta wasanii wa filamu nchini wenye heshima mimi huwezi kuniacha kwani najua silaha ya kuheshimika ni kujiepusha na wambeya ambao hutoa maneno huku na kupeleka kule, akili za kitoto nimeshaziacha na sasa ni mtu mzima na pia ninaitwa mama mtoto,” alisema Rose Ndauka.
Rose
alisema kitu kingine ambacho kinampa heshima katika jamii ni
uamuzi wa kumpenda kila mtu na kutokuwa na visasi na mtu
kwani wanadamu wote hawajakamilika hivyo ni vyema kusameheana
kila wanapokoseana.
0 Comments