Advertisement

Responsive Advertisement

NISHA WA BONGO MOVIE AFUNGUKA KUHUSU KUWA MJAMZITO

 
Mwanadada kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ 
MWANADADA kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amepangua madai kuwa ni mjamzito na kudai ni maneno ya ya watu licha ya kwamba ukikiangalia kwa makini kitumbo chake unaweza kuhisi kuna kitu ndani.

Akizungumzia madai hayo na kwamba ndicho kinachomfanya asijichanganye na wenzake kama kawaida, Nisha alisema kutoonekana kwake ni maamuzi tu. “Eti nina mimba!

Mh…nashangaa sana, sijui watu wanatoa wapi hayo maneno, mimi sina mimba na nilikuwa sionekani kwa sababu nilisafiri, pia mwezi mtukufu huwa sitoki hovyo, nikiamua kuzaa watu wataniona tu,” alisema Nisha.

Post a Comment

0 Comments