SHIRIKISHO la Soka wa
nchini-TFF limedai kutotambua mabadiliko ya uongozi ndani ya Coastal
Union yanayodaiwa kufanywa na mkutano wa wanachama wa klabu hiyo
uliofanyika hivi karibuni. Katika taarifa ya shirikisho hilo iliyotumwa
na Ofisa Habari wake Boniface Wambura, TFF imesema wao wanatambua
uongozi wa Coastal Union uliochaguliwa na mkutano wa uchaguzi wa klabu
na ndio wataendelea kufanya nao kazi, na sio uongozi mwingine wowote
ule. Shirikisho hilo limewakumbusha wanachama wakewakiwemo Coastal Union
kuheshimu katiba ya TFF pamoja na katiba zao, kwani hazitambui
mapinduzi ya uongozi wala kamati za muda za utendaji. TFF inafanya kazi
za kamati za utendaji zilizopatikana kwa njia ya uchaguzi tu. Taarifa
hiyo iliendelea kudai kuwa tayari TFF imepokea barua kutoka kwa Kaimu
Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mnguto ikilalamikia kusimamishwa
kwake na wanalifuatilia suala hilo kwa kina, na ikibainika kuwa kuna
viongozi wamehusika katika mapinduzi hayo watafikishwa katika vyombo
husika kwa hatua zaidi.
0 Comments