Wakati wewe ukipambana kuleta maridhiano
kila panapokuwa na migogoro inayohatarisha ustawi wa taifa, wengine
wanafanya njama za kukwamisha maridhiano na kukudhihaki. Ewe Rais
Kikwete, tenda wema nenda zako...... Mungu yuko upande wako na wenye
hekma wanakuelewa vyema na watakuwa wanashukuru kwa jitihada zako.
Wakati ukijishusha ili kutoa ushirikiano na kutoa mwanya watu watoe yao ya moyoni bila woga, wengine wanatumia mwanya huo kujikweza na kutaka kujionesha wao ni akina nani na ikibidi kuvuruga hali ya mambo ili ikibidi udhalilike. Ewe Rais, Kikwete, tenda wema nenda zako!
Wakati mataifa mengine na ulimwengu ukitambua mchango wako katika jamii, nyumbani wengi wanakubeza na kukukatisha tamaa, Ewe rais Kikwete, endelea na moyo wako wa kuwa mvumilivu na mtulivu wakati wote kwani wengi miongoni mwetu, katika yale yanayotokea, tungeweza kupata jazba na kufanya maamuzi ya hasira!.
Ewe rais Kikwete, Tenda wema nenda zako , wala usingoje shukurani kwani itakuletea matatizo. Mungu akujalie moyo mwepesi na utulivu kila unapokabiliana na changamoto kwa mambo yenye maslahi ya kitaifa na endelea kujishusha kwani kila anayejishusha basi huyo atakwezwa na kila anayejifaharisha ili watu wamjue yeye nani, hatimae atashushwa!.
Mungu akujaalie busara zaidi na hekma uweze kuendelea kuwa na moyo wa Ihsani.
Wachache wa kuelewa na waelewe, wale wa kuchanganyikiwa na wachanganyikiwe na wakutukana kwa sababu ya chuki nawatukane.

0 Comments