Kuna habari japo imewekwa kama tetesi,
ina ukweli kwamba CHADEMA wanatarajia kuitisha mkutano na waandishi wa
habari kuzungumzia sakata la bomu la soweto ambalo mpaka hivi leo hakuna
hatua yoyote iliyochukuliwa na serikali.
Inasemekana Mbunge wa Arusha
mjini atakuwepo kwenye press hiyo na waandishi wa habari, ambao watapewa
video hiyo kama ushahidi ili umma wa watanzania wauone mkanda ambao
utatoa taswira chanya kwa wananchi kujua ukweli kuhusu tukio lenyewe.
Habari ambazo zimepatikana ni kwamba
CHADEMA wataitisha mkutano na waandishi wa habari kabla ya kurusha video
ya bomu la soweto, ambalo lilionyesha wazi jinsi polisi walivyohusika
kutekeleza ulipuaji wa bomu.
Mkutano na waandishi wa habari unatarajiwa kuwa siku ya jumapili muda na mahali itatangazwa.
Tutaendelea ku update kadiri tutakavyokuwa tunapokea taarifa.
0 Comments