Ripoti kutoka Nigeria zinaeleza kuwa Jumamosi iliyopita kundi kubwa
la wanawake lilijitokeza na kuzuia magari ya jeshi yaliyokuwa yamewabeba
wanaume wao na wake zao yakielekea katika mji wa Gwosa, sehemu ambayo
inadhibitiwa na kundi la Boko Haram.
Kwa mujibu wa Prime Times ya Nigeria, wanawake hao walizua geti la
barracks katika mji wa Borno huku wengine wakilala barabarani
kushinikiza waume zao wapewe vifaa vya kisasa na imara zaidi ndipo
waende vitani kupambana na kundi hilo.
Hali hiyo imekuja baada ya kuripotiwa kuwa karibu wanajeshi 60
waliuawa Jumatano iliyopita katika eneo la Gwosa linalomilikiwa na Boko
Haram na kudaiwa kuwa sababu kubwa ni zana duni walizokuwa nazo
kulinganisha na zana za kisasa za kijeshi za kundi hilo.
Chanzo kimeiambia Prime Times kuwa wanawake hao walieleza kuwa
hawataki kubaki wajane na yatima kama wenzao kwa sababu ya vita hiyo.
“Mwanamke mmoja alisema ‘hatutaki kuwa kundi lingine la wajane,
wapeni waume zetu zana bora zaidi za kivita, silaha na magari bora zaidi
la sivyo hawaendi kokote’.”
Wanajeshi wengine pia walionekana kuunga mkono madai ya wanawake hao na kusukuma lawama kwa maafisa wa serikali.
“We are ever ready to tackle Boko Haram terrorists but our
superior officers are the ones killing us by not giving us the right
arms to execute the war. How could I go and face Boko Haram with AK47
that is charged with only three cartridges when the enemy is brandishing
modern GPMG, AA, RPG and so on.” Alikaririwa mwanajeshi mmoja.
Kundi la Boko Haram bado linawashikilia mateka wanafunzi wa kike
zaidi ya 200 na wanawake wengine huku likitekeleza mauaji ya kutisha
katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
You might also like:
0 Comments