Watu
wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia na kuwaua mume na mke na
kumjeruhi mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 4 aliyeachwa na mama yake
aliyeuawa katika tukio lililotokea kijiji cha Murvyagira wilayani Ngara
mkoani Kagera Ijumaa ya Agost 08,2014.
Kwa
mujibu wa mtoto mkubwa wa marehemu amesema majambazi hao walivamia
nyumbani kwao majira ya saa 3 usiku ambapo walitumia panga na jembe
kuwaua baba na mama yake na kisha kuwapora Maharage gunia moja, Radio,
Gunia la Karanga, Mabati na Fedha vitu ambavyo hadi sasa thamani yake
haijajulikana, huku wahalifu hao wakitokomea kusikojulikana.
Aidha
baadhi ya wananchi walioongea na mwandishi wetu, wameomba juhudi ya
kuimarishwa hali ya usalama na ulinzi wilayani Ngara izidishwe hasa
wakati huu ambako matukio ya mauaji yamezidi kujitokeza.
Mwili wa mwanaume ukiwa eneo la tukio baada ya kuuawa kwa kukatwa Mapanga na watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi.
Mwili
wa mwanamke ukiwa eneo la tukio baada ya kuuawa na majambazi hao.
Mama
huyo ameacha Mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 4 aliyejeruhiwa na watu
hao wanaodhaniwa ni majambazi.
0 Comments