Takribani wiki sasa kumekuwa na taarifa zinazoeleza kuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu hayuko sawa katika mahusiano yake ya kimapenzi na nguli wa Bongo Fleva, Diamond Plutnumz....
Kutokana
ta taarifa hizo, Mpekuzi iliamua kupekua undani wake na ndipo
ilipokutana na kilio kipya cha Wema Sepetu kuhusiana na
kuzushiwa taarifa mbalimbali asizozielewa chanzo chake....
Kwa
mujibu wa rafiki wa karibu na Wema, imefika mahali Wema
anajuta kuwa na Diamond kwa sababu ya kuandikwa kwa mambo
mengi yasiyo na ukweli na yanayomfedhehesha moyoni....
Rafiki
huyo amedai kuwa mara kwa mara Wema amekuwa akijiuliza sababu
ya kuandikwa taarifa mbalimbali zisizo na kichwa wala miguu
ambapo mwisho wa yote hupata jibu ni kwa sababu ya kuwa na
mahusiano na Diamond....
"Wakati
mwingine anasema angelijua bora angebaki bachela kwani kuna
kikundi cha watu hakipendi kumuona akiwa na Diamond hivyo
kinafanya kazi ya kumzushia taarifa zisizoeleweka kila mara kwa
lengo la kumshushia hadhi," kimesema chanzo hicho.
Mwandishi alipokiuliza chanzo hicho ni kwa kiasi gani Wema anamwamini Diamond kilisema:
"Ukweli
ni kwamba Wema anampenda sana Diamond lakini hamwamini kwa
sababu wakati mwingine taarifa zinazoandikwa magazeti hutolewa
na Diamond mwenyewe, hali hiyo inampa wakati mgumu sana Wema
kujua ashike wapi na wapi apaache,"
"Unajua Diamond haaminiki, unaweza kukuta Wema anagombana na watu kumbe mtoa taarifa ni Diamond mwenyewe."
0 Comments