Advertisement

Responsive Advertisement

ANGALIA PICHA_WAREMBO MISS TANZANIA 2014 WAWASILI KAMBINI, KANDA YA ZIWA WATINGA DAR NA GARI LAO LA USHINDI


Wanyange 30 wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2014 leo wameingia kambini tayari kwa safari ya fainali za Miss Tanzania 2014 zitakazo fanyikia mapema mwezi Oktoba jiji Dar es Salaam.

Warembo hao waliwasili kwa muda tofauti kuanzia saa 12 alfajiri ya leo na kupokelewa na waandaaji wa Miss Tanzania katika hoteli ya JB Belmont iliyopo katikati ya jiji la maraha la Dar. 

Warembo kutoka Kanda ya Ziwa walitia fora pale warembo hao walipowasili kambini hapo wakiwa ndani ya gari ya Mshindi wa Miss Kanda ya Ziwa 2014  alilozawadiwa hivi karibuni na Lenny Hotel ya mjini Geita

 Warembo wakiwasili kambini
Warembo hao wameanza kambi yao leo huku swali likibaki kwa mashabiki wa michezo wakisema kuwa kama Miss Lake Zone alipewa gari je Miss Tanzania atapewa nini?

Mmoja wa washabiki aliyejitmbulisha John Kisute mkazi mtaa wa Sinza alisema kuwa pamoja na yeye kupenda michezo na warembo wote 30 kuwa na mvuto wa aina yake lakini alikwenda kuangalia Gari alilokuwa anasikia limetolewa na Mkurugenzi wa Lenny Hotel kwani hakuamini kama ni kweli.
 Warembo wa Kanda ya Ziwa wakiteremka katika gari lao baada ya kuwasili na inaelezwa waliliendesha kutoka jijini Mwanza hadi Dar es salaam
 Warembo wa Kanda ya Ziwa wakijiandikisha baada ya kuwasili kambini.
 Warembo wakielekea chumba cha mkutano.
 Warembo wakiwa katika chumba cha semina ambapo maelezo mbalimbali ya kambi yao yalitolewa.
 Semina inaendelea
  Warembo wakiwa katika chumba cha semina ambapo maelezo mbalimbali ya kambi yao yalitolewa.
 Wadhamini wakijitambulisha kwa warembo na wanahabari.
 Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hasim Lundenga 'Anko' (kushoto) akiteta jambo na Katibu wake Bosco Majaliwa 'Mshua'.Lundenga alisema warembo hao wakiwa kambini hapo watatembelea vivutio mbalimbali na kujifunza mambo muhim ikiwemo  kutembelea kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Edward Moringe Sokoine
Chakula cha mchana kwa warembo.

Post a Comment

0 Comments