Staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe ‘Jack Wolper’
STAA
wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe ‘Jack Wolper’ amejikuta
akitumika kwenye utapeli wa mamilioni ya shilingi kupitia mitandao ya
kijamii bila yeye kujua,limeinyaka.
Akizungumzia sakata zima huku
alibubujikwa na machozi, Wolper alisema: “Siku moja nilikutana na dereva
teksi mmoja aitwaye Ismail, baada ya kupiga stori nilimpa namba yangu
ya simu na yeye akanipa yake, tukaagana.
“Siku chache baadaye Ismail akanipigia
simu na kuniuliza kulikoni naomba sana watu wanisaidie pesa kwenye
WhatsApp kwa ahadi ya kuwarejeshea?“Akaniambia kama nina tatizo bora
wakati mwingine nimshirikishe kuliko kila kukicha kuombaomba pesa.
“Hapo ndipo nikagundua kuna mtu
kajisajili kwa jina la Jacqueline Masawe na hata kwenye namba nyingine
za simu anazotumia kuomba watu pesa, amejisaliji kwa jina hilohilo.“Pia
kwenye Facebook, WhatsApp anatumia picha zangu, hapo ndipo nikagundua
kuwa, kuna mtu anatapeli watu kupitia jina langu,” alisema Wolper.
Staa wa filamu, ‘Jack Wolper’ akipozi.
Akaongeza kuwa, baada ya kugundua
utapeli huo akashangaa wanajitokeza watu wakisema wanamdai ambapo
imebainika mtu huyo alikuwa kakopa pesa kwa watu tofauti zinazofikia
shilingi milioni 10 lakini wengi walimuelewa hivyo kuripoti tukio hilo
kwa vyombo vinavyohusika ili kumsaka mtuhumiwa.
0 Comments