Watu
kumi wamefariki dunia baada ya kukakanyagwa na gari lililokuwa
linakwenda kwa mwendo wa kasi walipokuwa wanajaribu kujipatia angalau
kipande cha nyama ya Kiboko mwishoni mwa wiki.
Kiboko huyo alikuwa
amegongwa na gari na kufariki Jumamosi jioni katika mkoa wa Limpopo
nchini Afrika Kusini wakati ambapo wanakijiji walikimbia katika sehemu
hiyo angalau kujipatia kipande cha nyama.
Msemaji wa polisi
aliambia shirika la habari la AFP kwamba mnyama huyo aligongwa na
wanakijiji wakaona fursa ya nyama ya bure ambapo walikimbia kuinyakua na
kuanza kuikatakata, ''
''Hapo ndipo gari
lililokuwa linakwenda kwa kasi liliwagonga watu 8 walipokuwa wanakata
nyama hiyo na kuwaua,'' aliongeza kusema msemaji huyo wa polisi.
Watu wengine wawili walifariki kutokana na majereha yao mabaya wakiwa wanapokea matibabu hospitalini.
Polisi wanasema kuwa watu wengine saba akiwemo dereva wa gari hilo wanapokea matibabu hospitalini.