Mkurugenzi mkuu wa FBI James Comey
amesema kitengo chake kimemtambua mtu ambaye huficha sura yake ambaye ni
muuaji,ambaye pia huoneshwa wakati akiwachinja mateka watatu kwenye
video inayo nadi wanamgambo wa dola ya kiislam IS.
Pamoja na hayo
Bwana Comey amegoma kuutaja uraia wa mtu huyo ama hata kutaja jina
lake,ingawa imeshajulikana lafudhi ya mtu huyo kuwa ni mwenye asili ya
mji wa London, na Comey amesema kwamba utambuzi wa mtu huyo
umefanikishwa kwa msaada mkubwa wa marafiki wa kimataifa.
Muuaji
huyo wa waandishi James Foley na Steven Sotloff pamoja na mfanyakazi wa
kujitolea David Haines walipigwa picha ya video na kuwekwa kwenye
mitandao na wanamgambo hao wa dola ya kiislam na kusaidia kufanya
maamuzi juu ya mipango ya wapiganaji wa jihad.
0 Comments