Baraza la wanawake la Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA nchini
Tanzania BAWACHA limeandaa maandamano kwa wanawake ambayo yanalenga
kumuomba Rais Jakaya Kikwete kutosaini rasimu ya katiba kwa madai kwamba
itakuwa haijapatikana kama wananchi walivyotarajia
Mwenyekiti
wa BAWACHA na Mbunge wa jimbo la Kawe Halima Mdee amesema maandamano
hayo yatafanyika baada ya wiki moja kuanzia sasa na kwamba yanalenga
kuhakikisha rasimu hiyo ya katiba inapatikana kwa kutokana na michango
ya mawazo kwa pande zote na vyama vyote vilivyopo kisheria.
Mdee amesema maandamano hayo hayatahusisha wanawake wa chama hicho pekee bali yatahusisha pia wanawake kutoka maeneo yote ya jiji kwa lengo la kufikisha ujumbe husika .
Mdee amesema maandamano hayo hayatahusisha wanawake wa chama hicho pekee bali yatahusisha pia wanawake kutoka maeneo yote ya jiji kwa lengo la kufikisha ujumbe husika .
You might also like:
0 Comments